Msimu huu namba za Yanga zinakataa, mtihani uko hapa!
NAMBA ambazo Yanga walizitengeneza msimu uliopita wa ligi 2024-2025, zinaonekana kuwakimbia msimu huu wa 2025-2026 na watatakiwa kufanya kazi ya ziada ili kuzifikia huku mambo yakionekana kutowaendea vizuri. Yanga ambao wamemaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara wakiwa kileleni, jana walianza mzunguko wa pili kwa kuambulia sare ya bao 1-1 dhidi ya Mtibwa Sugar…