SOUWASA YATOA TUZO KWA WATEJA KINARA WA MALIPO YA ANKARA ZA MAJI.
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Songea (SOUWASA) imewatunukia tuzo wateja wake kinara katika makundi matatu ambayo ni majumbani, maeneo ya biashara na taasisi pamoja na Tuzo maalumu kwa mdau anashirikiana bega kwa bega na Mamlaka kwenye utoaji taarifa na ushauri, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha ulipaji wa bili kwa wakati na kuboresha ushirikiano…