Nchimbi: Magufuli ameacha darasa la uongozi
Dar es Salaam/Chato. Makamu wa Rais, Dk Emmanuel Nchimbi amesema maisha na uongozi wa Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli yalikuwa darasa muhimu kwa viongozi na Watanzania kwa ujumla, akisisitiza kuwa namna bora ya kumuenzi ni kuishi na kutenda yale aliyoyaamini. Nchimbi ameyasema hayo leo Machi 17, 2026 alipozungumza baada ya misa takatifu…