Moto wateketeza kiwanda cha rasta Buguruni Sukita, juhudi kuuzima zinaendelea
Dar es Salaam. Moto ambao chanzo chake bado hakijajulikana unaendelea kuwaka katika kiwanda kinachojishughulisha na uzalishaji wa nywele bandia, maarufu rasta kilichopo eneo la Buguruni Sukita, Wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam. Kwa mujibu wa mashuhuda moto huo umeanza usiku wa kuamkia leo Jumanne, Machi 17, 2026 na kuzua taharuki kwa wafanyakazi na watu…