Polisi Watoa Onyo Dhidi ya Uzushi wa ‘Kuibiwa Nyeti’ Mitandaoni – Video

Global Publishers
April 6, 2026
0 Comments

Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime

Jeshi la Polisi limetoa onyo kwa wote wanaosambaza uzushi mitandaoni kuhusu ‘kuibiwa nyeti’ na kueleza kuwa watasakwa na kukamatwa.

Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime amesema taarifa potofu za madai kuwa mwanaume akiguswa begani, nyeti zinapotea kimazingara hazina ukweli wowote na kueleza kuwa zimesababisha watu saba kuuawa mpaka sasa.

🔴 Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV, like, comment ili kuendelea kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.