Urithi utakaokumbukwa kwa Karume | Mwananchi
Dar es Salaam. Leo ni miongo mitano na miaka minne tangu alipotwaliwa Rais wa kwanza wa Zanzibar, Sheikh Abeid Amani Karume, huku wadau wa siasa wakimkumbuka kwa misingi aliyoiasisi, ambayo baadhi wanadai imeachwa. Karume alifariki dunia Aprili 7, 1972, baada ya kupigwa risasi Kisiwandui, Unguja, visiwani Zanzibar, zilipokuwa ofisi za Makao Makuu ya Chama cha…