Global Publishers
April 7, 2026
0 Comments
Staa wa reality TV Kim Kardashian na bingwa wa dunia wa Formula One, Lewis Hamilton, hatimaye wameweka wazi uhusiano wao hadharani kupitia mtandao wa Instagram.
Wawili hao walithibitisha penzi lao Aprili 6 baada ya Hamilton kushare video (Reel) ikimuonesha akiwa na Kardashian ndani ya gari kali aina ya Ferrari F40 wakifanya mizunguko ya kasi (donuts) katika eneo maarufu la Daikoku Parking Area jijini Tokyo.
Katika video hiyo, Kardashian anaonekana akiwa siti ya abiria huku akishangazwa na mwendo wa kasi wa Hamilton, akisema, “That’s insane,” akimaanisha tukio hilo lilikuwa la kusisimua sana.

Hamilton aliambatanisha video hiyo na maneno: “HERE WE GO AGAIN 🇯🇵 TOKYO DRIFT VOL. III,” ishara kuwa hii si mara yao ya kwanza kufurahia maisha pamoja nchini Japan.
Taarifa zinaeleza kuwa kabla ya kuweka wazi uhusiano huo, wawili hao walikuwa tayari wakionekana pamoja Tokyo wakipumzika, ambapo Kardashian aliambatana na watoto wake aliopata na rapa Kanye West. Pia dada yake, Khloé Kardashian, alikuwepo katika safari hiyo.
Chanzo cha karibu kimeeleza kuwa Hamilton amepokelewa vizuri na familia ya Kardashian, huku akielezewa kuwa mtu mcheshi na mwenye nishati chanya.
Inaelezwa pia kuwa uhusiano wao si wa kawaida tu, kwani wote wawili wanaonekana kuwa na hisia za dhati licha ya ratiba zao kuwa na shughuli nyingi.
Uvumi wa penzi lao ulianza kushika kasi mwezi Machi baada ya Hamilton kuacha emoji ya mapenzi kwenye picha ya Kardashian aliyoiweka Instagram kitu kilichoibua mjadala mkubwa mtandaoni.
Sasa, kwa kuweka wazi mahusiano yao hadharani, ni wazi kuwa wawili hao hawafichi tena hisia zao.