BARRICK YAPOKEA UAMUZI WA MAHAKAMA YA RUFAA YA ONTARIO WA KUTUPILIA MBALI RUFAA KUHUSU MGODI WA NORTH MARA

Kampuni ya Barrick Mining Corporation imepokea uamuzi wa Mahakama ya Rufaa ya Ontario kutupilia mbali rufaa ya baadhi ya wakazi wa Tanzania wanaodai kuwepo ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na askari wa Jeshi la Polisi la Tanzania karibu na mgodi wa dhahabu wa Kampuni ya North Mara.

Uamuzi huu uliunga mkono uamuzi wa awali wa Mahakama ya Juu ya Ontario ambayo iligundua kuwa Ontario sio jukwaa mwafaka la kushughulikia madai haya na kwamba ni lazima yahukumiwe nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliotolewa nchini Canada imebainisha kuwa Ushahidi uliowasilishwa wakati wa kesi hii ulithibitisha kwamba Jeshi la Polisi la Tanzania linafanya kazi bila ya kutegema Barrick, ambayo inashikilia sera ya kutovumilia ukiukwaji wa haki za binadamu kwa wafanyakazi, wakandarasi au wahusika wengine wanaofanya kazi kwa niaba yake.

Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Hill, alisema: “Barrick inajivunia kazi yetu nchini Tanzania, ambayo tunaifanya kwa ushirikiano wa karibu na ngazi zote za serikali pamoja na jamii zinazotuzunguka.

Kazi yetu kwa pamoja inazalisha ajira, inachochea maendeleo ya kiuchumi na kuboresha maisha ya Watanzania wengi.”

Kuhusu Barrick Mining Corporation

Barrick ni kampuni inayoongoza duniani ya uchimbaji madini, utafii na maendeleo. Ikiwa na mojawapo ya hazina kubwa zaidi za ubora wa dunia na rasilimali za kudumu muda mrefu za dhahabu na shaba katika sekta hii, shughuli na miradi ya Barrick inahusisha nchi 17 na mabara matano. Barrick pia ni mzalishaji mkubwa wa dhahabu nchini Marekani. Tunaunda thamani halisi, ya muda mrefu kwa washikadau wote kupitia uchimbaji madini unaowajibika, ushirikiano thabiti na mbinu yenye nidhamu ya ukuaji. Barrick inashiriki biashara kwenye Soko la Hisa la New York chini ya alama ya ‘B’ na kwenye Soko la Hisa la Toronto chini ya nembo ya ‘ABX’.