Bakari Mahundu
April 8, 2026
0 Comments
Kama sehemu ya maadhimisho ya sikukuu ya Pasaka kote nchini, Serengeti Apple iliandaa premium brunch experience maalum mwishoni mwa wiki katika hoteli ya Serena Hotel Dar es Salaam, ikiwapatia wageni waalikwa uzoefu wa kipekee ulioendana na shamrashamra za sikukuu hiyo.
Likiwa limeandaliwa katika mazingira ya kifahari yenye mandhari tulivu na mpangilio wa kisasa, tukio hilo lilijumuisha vipengele mbalimbali ikiwemo mazungumzo ya karibu, burudani nyepesi ya muziki pamoja na huduma ya kiwango cha juu. Uzoefu huo ulikamilishwa na ladha ya kipekee na ya kuburudisha ya Serengeti Apple—kinywaji kinachozalishwa na Serengeti Breweries Limited hapa nchini.

Kuanzia mapambo ya meza hadi vibe ya tukio zima, kila kipengele kilizingatia ubora na umakini wa hali ya juu, kikitoa taswira halisi ya namna sikukuu na matukio ya kijamii yanavyoweza kusherehekewa kwa mtindo wa kisasa na wa kifahari.

Kupitia uzoefu huu, Serengeti Apple inaendelea kujijengea nafasi kama kinywaji kinachoendana na matukio ya kijamii yenye hadhi, kwa kuunganisha ladha, mazingira na mtindo wa maisha wa kisasa.

#SerengetiApple #ProudlyTanzanian