Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Uvuvi Prof. Mohammed Sheikh,akizungumza leo Aprili 8,2026 wakati akizindua mafunzo ya siku tano kwa maafisa wakaguzi wa mazao ya uvuvi 25 yaliyoandaliwa na Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) kwa kushirikiana na Shirika la Kilimo na Chakula Duniani (FAO).
…..
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Uvuvi Prof. Mohammed Sheikh amewataka wakaguzi wa mazao ya uvuvi kufanya kazi zao kwa ubora ili kulisaidia Taifa kuongeza kiwango cha mazao ya uvuvi yanayosafirishwa nje ya nchi.
Prof Sheikh ametoa kauli hiyo 8 April, 2026 wakati akizindua mafunzo ya siku tano kwa maafisa wakaguzi wa mazao ya uvuvi 25 yaliyoandaliwa na Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) kwa kushirikiana na Shirika la Kilimo na Chakula Duniani (FAO).
“Takwimu zinaonesha kwasasa tunasafirisha tani 60,000 pekee za samaki kwenda nje ya nchi hivyo uwepo wa mafunzo haya uwe chachu ya kuongeza ubora utakaosaidia Taifa kuongeza kiasi cha samaki kinachopelekwa nje ya nchi” Amesema Prof. Sheikh
Kwa uoande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) Dkt Semvua Mzighani amesema Mafunzo haya yamelenga kuwajengea uwezo maafisa ukaguzi wa mazao ya uvuvi juu ya taratibu za ukaguzi wa mazao ya uvuvi pamoja na viwango vya ubora vya kitaifa,kikanda na kimataifa.
Pia amewasihi washiriki wa mafunzo kuzingatia mafunzo watakayopatiwa na elimu watakayoipata kupitia mafunzo hayo ikawasaidie wananchi katika maeneo yao.
Awali Mratibu wa mafunzo hayo Mkufunzi Anold Mbunda amesema hii ni awamu ya kwanza ya mafunzo ambapo imejumuisha washiriki toka ukanda wa pwani, awamu ya pili ya mafunzo haya itafanyika mkoani Kigoma ambapo itahusisha washiriki kutoka kanda ya ziwa.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Uvuvi Prof. Mohammed Sheikh,akizungumza leo Aprili 8,2026 wakati akizindua mafunzo ya siku tano kwa maafisa wakaguzi wa mazao ya uvuvi 25 yaliyoandaliwa na Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) kwa kushirikiana na Shirika la Kilimo na Chakula Duniani (FAO).

Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) Dkt Semvua Mzighani,akizungumza wakati wa mafunzo ya siku tano kwa maafisa wakaguzi wa mazao ya uvuvi 25 yaliyoandaliwa na Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) kwa kushirikiana na Shirika la Kilimo na Chakula Duniani (FAO).

Sehemu ya washiriki wakifatilia hotuba ya Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Uvuvi Prof. Mohammed Sheikh (hayupo pichani) ,wakati akizindua mafunzo ya siku tano kwa maafisa wakaguzi wa mazao ya uvuvi 25 yaliyoandaliwa na Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) kwa kushirikiana na Shirika la Kilimo na Chakula Duniani (FAO).

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Uvuvi Prof. Mohammed Sheikh,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua mafunzo ya siku tano kwa maafisa wakaguzi wa mazao ya uvuvi 25 yaliyoandaliwa na Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) kwa kushirikiana na Shirika la Kilimo na Chakula Duniani (FAO).