Video: Rais Samia Aelekeza Serikali Kupunguza Matumizi ya Mafuta

Global Publishers
April 8, 2026
0 Comments

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza mara baada ya kuwaapisha Viongozi Wateule, Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 08 Aprili, 2026.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametoa onyo kwa wafanyabiashara nchini dhidi ya kutumia mwanya wa kupanda kwa bei ya mafuta kupandisha bei za bidhaa kupita kiasi, akisisitiza umuhimu wa kuzingatia uhalisia wa gharama za uendeshaji.

Akizungumza leo Jumatano, Aprili 8, 2026, Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma wakati wa kuwaapisha viongozi wapya aliowateua, Rais Samia amesema:

“Isitumike fursa ya kupanda kwa mafuta na kuweka bei za bidhaa kubwa kuliko zinavyopaswa kuwa. wananchi, kuna bidhaa ambazo zinaingia kipindi hiki ambazo zimekumbana na msukosuko huu zitapanda bei.”

Amefafanua kuwa ongezeko la bei ya mafuta linatokana na hali ya soko la kimataifa na si maamuzi ya Serikali ya Tanzania, huku akibainisha kuwa bado bei ya mafuta nchini iko chini ukilinganisha na mataifa mengine.

Kauli hii inalenga kudhibiti hali ya baadhi ya wafanyabiashara wanaoweza kutumia changamoto ya mabadiliko ya bei ya mafuta kama kigezo cha kuongeza bei zisizo na uwiano, jambo ambalo linaweza kuathiri wananchi moja kwa moja kupitia ongezeko la gharama za maisha.