Global Publishers
April 9, 2026
0 Comments
Wabunge wateule wawili, Angela Kizigha na Evaline Munisi, leo Aprili 09, 2026 wamekula kiapo cha uaminifu na ahadi ya uzalendo Bungeni jijini Dodoma.
Hafla hiyo imefanyika ikiwa ni hatua rasmi ya kuanza majukumu yao ya uwakilishi baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.
Wabunge hao wameahidi kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, kuzingatia Katiba ya nchi pamoja na kuwatumikia wananchi kwa uaminifu na uzalendo katika kipindi chao cha uongozi.

