………
Na Ester Maile Dodoma
Taasisi ya Moyo ya Jakaya kikwete imeandaa kampeni ya ijue namba yako ,kwa lengo la kuwataka wananchi kùweza kujua mapigo yao ya moyo ,sukari ,na mafuta yaliyopo mwilini kwa kupima afya zao mara kwa mara na kufanya mazoezi ili kupunguza changamoto la tatizo la moyo .
Amezungumza hayo Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo Dk. Peter Kisenge wakati akizungumza na waandishi wa habari leo 9 Aprili jijini Dodoma wakati akitoa mafanikio yaliyopo katika taasisi hiyo.
Aidha Dk Kisenge amesema vifo vingi vinavyotokea vinatokana na tatizo la moyo ambapo kwa asilimia kubwa linawapata wanaume huku ikielezwa chanzo kikubwa ni mitindo wa maisha,huku akitaja uvutaji wa sigara na sisha kusababisha tayizo hilo.
Hata hivyo taasisi ya Moyo ya Jakaya kikwete imeandaa mfumo maalumu wa upandikizaji wa moyo ambapo itaenda kuokoa maisha ya watanzania wengi .




