MWENYEKITI NYAMKA ATUA RASMI KATA YA MBWAWA AWAHIMIZA WANA CCM KUKIIMARISHA CHAMA

VICTOR MASANGU,KIBAHA .

Chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha  mjini imewapongeza kwa dhati wanachama wake na wananchi kwa ujumla kwa kuweza kukipa kura nyingi za kishindo wakati  wa uchaguzi mkuu uliofanyika octoba 29 mwaka 2026.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa chama hicho Mwalimu Mwajuma Nyamka wakati wa ziara maalumu ambayo imeanza leo rasmi katika kata ya Mbwawa yenye lengo  kubwa la kuwashukuru wanachama pamoja na wanannchi.

Katika ziara hiyo ambayo imehudhuliwa na viongozi mbali mbali wa chama hicho pamoja na baadhi ya viongozi wa  jumuiya ya Wazazi,pamoja na jumuiya ya umoja wa wanawake wa (UWT) Kibaha mjini wameweza kuwatembelea  na kuzungumza na baadhi ya mabalozi wa matawi Kata ya Mbwawa.

Mwenyekiti Nyamka amesema kwamba pamoja na ziara hiyo kulenga kutoa shukrani pia ameanbatana na baadhi ya wataalamu kutoka Ofisi ya vizazi na vifo Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha (Rita) kwa  lengo la kuwasaidia wananchi wenye changamoto ya ukosefu wa vyeti vya kuzaliwa.

“Mimi kama mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM)  Wilaya ya Kibaha mjini pamoja na  viongozi wenzangu tumeanza ziara rasmi ya kuwashukuru wanachama pamoja na wananchi kwa ajili ya kutoa pongezi na shukrani kwa kukipigania chama kushi da  kwa kishindo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2026,”amesema Mwenyekiti Nyamka.

Nyamka amebainisha kwamba   amefarijika sana na kitendo cha wanachama wa ccm sambamba na wananchi wote kuweza kupambana na kuchagua mafiga matatu kwa kishindo  katika nafasi ya udiwani,ubunge,pamoja na kiti cha Urais.

Kadhalika amewahimiza wanachama kuendelea kushikamana  kwa kishindo kuanzia ngazi za chini lengo ikiwa ni kuweza kukiimarisha chama ikiwa pamoja na kutekeleza ilani kwa vitendo.

Nao baadhi ya viongozi mbali mbali wa mashina wakizungumza kwa nyakati tofauti wamempongeza kwa dhati Mwenyekiti wa CCM Mwalimu Mwajuma Nyamka kwa kuweza kufanya ziara hiyo  na kwenda kuwatembelea na kuwajulia hali zao.

Mmoja wa balozi kutoka Mbwawa shule shina namba  nne Ramadhani Chuma alikishukuru chama chake kwa kuweza kuona umuhimu mkubwa wa kwenda nyumbani kwake kumtembelea kitendo ambacho kimeweza kumfariji sana.

ZIara ya Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mjini Mwalimu Mwajuma Nyamka imeanza leo rasmi katika kata ya Mbwawa ambapo imetembelea baadhi ya viongozi wakiwemo mabalozi pamoja na kufanya mkutano wa hadhara kwa lengo la kuwashukuru wanachama na wananchi.