Serikali Yatoa Ufafanuzi Kupanda Kwa Bei za Mafuta Duniani – Video

Global Publishers
April 9, 2026
0 Comments

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa.

Aprili 08, 2026 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, wakati akiwaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni, alizungumzia changamoto ya kupanda kwa bei za mafuta duniani, jambo lililozua maswali kwa baadhi ya wananchi.

Katika ufafanuzi wa kauli hiyo, imeelezwa kuwa:

  • Bei ya mafuta ya dizeli katika soko la dunia imeongezeka kwa dola za Marekani 800 kwa tani, ikitoka dola 650 mwezi Februari 2026 hadi kufikia dola 1,450 mwezi Machi 2026.
  • Bei ya petroli imeongezeka kwa dola 434 kwa tani, kutoka dola 618 mwezi Februari hadi dola 1,052 mwezi Machi 2026.
  • Bei ya mafuta ya taa pamoja na mafuta ya ndege imeongezeka kwa dola 821 kwa tani, kutoka dola 679 hadi dola 1,500 kwa kipindi hicho hicho.

Licha ya ongezeko hilo kubwa la bei kimataifa, Tanzania bado inaendelea kuwa na viwango vya chini vya bei za mafuta ukilinganisha na baadhi ya nchi nyingine duniani.

Sababu kuu ya kupanda kwa bei hizo imetajwa kuwa ni athari za mvutano wa kijeshi kati ya Iran, Israel na United States, hali iliyosababisha kufungwa kwa lango muhimu la mafuta duniani la Strait of Hormuz. Njia hiyo ni muhimu kwa usafirishaji wa mafuta kwenda sehemu mbalimbali duniani, ikiwemo Afrika.