KONA YA MSTAAFU: Sh5.5 milioni zipate ‘uteuzi’ wa dharura kwa wastaafu!
Kibubu cha akiba ya wafanyakazi, ambacho kimemtunzia akiba yake kwa miaka 40 ya ajira, huyu mstaafu, kimefanya kile kinachoamini kuwa ni bonge la kuboresha maisha ya huyu mstaafu, ili aweze kukabiliana na hali ngumu ya maisha, hususan tangu alipostaafu na kuambiwa sasa matibabu ya dezo kwa wazee ni maneno ya kanga tu! Kibubu kinajifagilia kwamba…