Fahamu Majukumu ya Rais wa Iran na Kiongozi Mkuu Mojtaba Khamenei

Ayatollah Mojtaba Khamen

Mfumo wa uongozi wa Iran ni wa kipekee ukilinganisha na nchi nyingi duniani. Nchi hiyo ina viongozi wawili wakuu wenye majukumu tofauti lakini yanayohusiana kwa karibu:

Rais na Kiongozi Mkuu wa Taifa (Supreme Leader). Ingawa wote wana nafasi muhimu katika uendeshaji wa nchi, mamlaka yao yanatofautiana kwa kiwango kikubwa.

Kiongozi Mkuu wa Iran, anayejulikana kama Supreme Leader of Iran, ndiye mwenye mamlaka ya mwisho katika masuala yote ya nchi.

Kwa sasa nafasi hii inashikiliwa na Ayatollah Mojtaba Khamenei baada ya baba yake Ayatollah Ali Khamenei kuuawa kwenye shambulio lililotekelezwa kwa ushirikiano wa Israel na Marekani.

Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian

Kiongozi Mkuu ndiye anayesimamia mwelekeo wa taifa kwa ujumla, kuanzia siasa, uchumi, hadi masuala ya ulinzi na usalama. Pia ndiye mkuu wa majeshi yote ya nchi, akitoa maamuzi ya mwisho kuhusu operesheni za kijeshi.

Mbali na hilo, ana mamlaka ya kuteua viongozi wa taasisi muhimu kama vile mahakama, vyombo vya usalama, na hata baadhi ya nafasi nyeti za kisiasa.

Kwa kifupi, Kiongozi Mkuu ndiye nguzo kuu ya uongozi wa Iran, na maamuzi yake yana uzito wa mwisho katika masuala makubwa ya taifa.

Rais wa Iran: Kiongozi wa Serikali Kwa upande mwingine, Rais wa Iran ndiye kiongozi wa serikali anayeshughulikia shughuli za kila siku za utawala. Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian

Rais huchaguliwa na wananchi kupitia uchaguzi, na jukumu lake kuu ni kusimamia utekelezaji wa sera za serikali. Hii ni pamoja na kuongoza baraza la mawaziri, kusimamia uchumi, kuboresha huduma za jamii, na kuiwakilisha Iran katika jukwaa la kimataifa.

Hata hivyo, pamoja na majukumu hayo, Rais hana mamlaka ya mwisho katika masuala makubwa ya taifa. Maamuzi Tofauti kubwa kati ya Rais na Kiongozi Mkuu iko katika kiwango cha mamlaka.

Wakati Rais anahusika zaidi na utekelezaji wa sera na uendeshaji wa serikali, Kiongozi Mkuu ndiye anayetoa mwelekeo wa jumla wa nchi na kuwa na neno la mwisho katika maamuzi muhimu.

Aidha, Rais huchaguliwa na wananchi moja kwa moja, ilhali Kiongozi Mkuu hachaguliwi kwa njia hiyo bali huteuliwa kupitia mfumo maalum wa kidini na kisiasa.

Mfumo wa uongozi wa Iran unaonyesha mchanganyiko wa siasa na dini, ambapo mamlaka ya juu yapo mikononi mwa Kiongozi Mkuu, huku Rais akibeba jukumu la kusimamia utekelezaji wa sera za serikali. Hali hii inaifanya Iran kuwa na mfumo wa kipekee unaotofautiana na mifumo ya uongozi ya nchi nyingi duniani.