Nafasi za Kazi 6 kwa Madereva Zatangazwa Shinyanga, Maombi Mwisho Aprili 15

Global Publishers
April 10, 2026
0 Comments

Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga inawatangazia Watanzania wenye sifa kuomba nafasi za kazi sita (06) za Dereva Daraja la II, baada ya kupata kibali kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

1.0 NAFASI ZINAZOTANGAZWA

Dereva Daraja la II – Nafasi 06

1.1 MAJUKUMU YA KAZI

Mwombaji atakayefanikiwa ataweza:

  • Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama
  • Kuwasafirisha watumishi kwenda maeneo mbalimbali ya kikazi
  • Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari
  • Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali
  • Kujaza na kutunza taarifa za safari (log book)
  • Kufanya usafi wa gari
  • Kutekeleza majukumu mengine atakayopangiwa na msimamizi wake

1.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Mwombaji anapaswa kuwa na:

  • Elimu ya Kidato cha Nne (Form IV)
  • Leseni ya Daraja C au E ya uendeshaji magari
  • Uzoefu wa kuendesha gari kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali
  • Cheti cha mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Course) kutoka VETA au chuo kinachotambuliwa na Serikali

1.3 NGAZI YA MSHAHARA

1.4 MASHARTI YA JUMLA YA MWOMBAJI

  • Awe raia wa Tanzania mwenye umri wa miaka 18 hadi 45
  • Aambatanishe CV kamili (Detail Curriculum Vitae) yenye:
    • Anwani ya makazi
    • Namba za simu zinazopatikana
    • Barua pepe (E-mail address)
    • Majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika
  • Aambatanishe nakala za vyeti vya elimu na taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili
  • Result slips (Form IV & Form VI) hazitakubaliwa
  • Vyeti vya wahitimu wa nje ya nchi lazima viidhinishwe na TCU, NECTA au NACTE
  • Waombaji waliostaafu utumishi wa umma hawaruhusiwi kuomba bila kibali maalum
  • Waombaji waliopo kwenye ajira za umma wanapaswa kufuata Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010
  • Uwasilishaji wa taarifa za kughushi utachukuliwa hatua za kisheria
  • Ni waombaji watakaokidhi vigezo pekee ndio watakaoitwa kwenye usaili

1.5 JINSI YA KUTUMA MAOMBI

Maombi yote yawasilishwe kupitia mfumo wa kielektroniki wa ajira (Recruitment Portal) kwa kutumia:
👉 https://portal.ajira.go.tz/

1.6 MWISHO WA KUTUMA MAOMBI

📅 15 Aprili, 2026

1.7 MAELEKEZO YA ZIADA

Mwombaji anatakiwa kuambatisha barua ya maombi iliyosainiwa pamoja na vyeti vyake. Barua ielekezwe kwa:

Mkurugenzi wa Manispaa
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
S.L.P. 28
SHINYANGA

Soma zaidi hapa >> NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA MANISPAA YA SHINYANGA 08-04-2026