Global Publishers
April 10, 2026
0 Comments
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amewakutanisha na kuwapatanisha waimbaji wa muziki wa injili, Martha Mwaipaja na Upendo Nkone, waliokuwa na tofauti kwa muda.
Hatua hiyo imekuja baada ya kuwepo kwa mvutano uliokuwa ukizungumzwa katika mitandao ya kijamii na miongoni mwa mashabiki wao, hali iliyokuwa ikizua mjadala katika tasnia ya muziki wa injili nchini.
Kupitia kikao hicho cha maridhiano, pande zote mbili zimefanikiwa kuweka kando tofauti zao na kurejesha mahusiano, hatua inayotajwa kuwa muhimu kwa kudumisha umoja na mshikamano katika sanaa ya injili.
Hatua ya Chalamila imepongezwa na wadau mbalimbali wakisema imeonesha umuhimu wa viongozi kushiriki katika kutatua migogoro ya kijamii kwa njia ya amani na maelewano.