Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Dkt. Fabian Madele, akihutubia wadau mbalimbali wa Sekta ya Mifugo, wakati wa warsha ya utambulisho wa Mradi wa Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT) ya Unenepeshaji wa Mbuzi na Kondoo, uliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) – Kongwa, Aprili 9, 2026 Dodoma.

Mtaalam wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Mradi wa Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT) ya Unenepeshaji wa Mbuzi na Kondoo, ambaye ni Mchumi Mwandamizi Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), Bw. Tumsime Mutta (aliyesimama), akielezea Mpango Mkakati wa Mradi, wakati wa warsha ya utambulisho wa Mradi huo, uliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) – Kongwa, Aprili 9, 2026 Dodoma.

Mtaalam wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Mradi wa Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT) ya Unenepeshaji wa Mbuzi na Kondoo, ambaye ni Mchumi Mwandamizi Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), Bw. Tumsime Mutta (aliyesimama), akielezea Mpango Mkakati wa Mradi, wakati wa warsha ya utambulisho wa Mradi huo, uliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) – Kongwa, Aprili 9, 2026 Dodoma.

Mchungaji wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ndg. Jeremia Nyato (aliyesimama), akitoa Ushauri wa namna ya kuwashawishi vijana kukimbilia fursa za unenepeshaji Mifugo, wakati wa warsha ya utambulisho wa Mradi wa Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT) ya Unenepeshaji wa Mbuzi na Kondoo, uliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) – Kongwa, Aprili 9, 2026 Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Dkt. Fabian Madele (katikati), akijibu hoja mbalimbali za wadau wa Sekta ya Mifugo, wakati wa warsha ya utambulisho wa Mradi wa Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT) ya Unenepeshaji wa Mbuzi na Kondoo, uliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) – Kongwa, Aprili 9, 2026 Dodoma, kulia ni Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa ambaye ni Afisa Tarafa ya Kongwa, Bw. Jerimia.

Picha ni baadhi ya wadau wa Sekta ya Mifugo wakimsikiliza Mgeni Rasmi ambaye ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Dkt. Fabian Madele (hayupo pichani), wakati wa warsha ya utambulisho wa Mradi wa Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT) ya Unenepeshaji wa Mbuzi na Kondoo, uliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) – Kongwa, Aprili 9, 2026 Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Dkt. Fabian Madele (aliyekaa katikati), akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa Sekta ya Mifugo, wakati wa warsha ya utambulisho wa Mradi wa Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT) ya Unenepeshaji wa Mbuzi na Kondoo, uliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) – Kongwa, Aprili 9, 2026 Dodoma.
….
Wizara ya Mifugo na Uvuvi inayotekeleza Mradi wa miaka mitano wa Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT) ya Unenepeshaji wa Mbuzi na Kondoo katika eneo la Kituo cha Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) iliyopo Wilayani Kongwa, imepanga kuwawezesha vijana 200 wa Kitanzania kupata Mafunzo hayo ikiwa na lengo la kuongeza ushiriki wa vijana na wanawake katika ujasiliamali wa Biashara ya Mifugo.
Akizungumza leo Aprili 9, 2026 Wilayani Kongwa Jijini Dodoma kwa Niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, wakati wa warsha ya utambulisho wa Mradi huo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Dkt. Fabian Madele, amesema mradi huo wenye thamani ya takribani shilingi Billioni 81, unalenga kuwawezesha vijana kupitia shughuli za unenepeshaji wa mbuzi na kondoo kibiashara, uzalishaji wa malisho na mbegu za malisho, uchakataji wa vyakula vya mifugo, pamoja na matumizi ya teknolojia za kisasa.
“Walengwa wakuu wa mradi huu ni vijana, ambao kupitia utekelezaji wake watapata ujuzi na uzoefu wa vitendo katika mnyororo mzima wa thamani wa mazao ya mifugo, hususan mbuzi, na kupitia mafunzo haya, vijana wetu watajengewa uwezo wa kuingia kwenye biashara za kisasa za mifugo na hivyo kujiongezea kipato pamoja na kuchangia ukuaji wa uchumi wa taifa.” Amesema Dkt. Madele
Aidha, Dkt. Madele amesema baada ya vijana kupata ujuzi huo, matarajio ya Serikali ni kuwa vijana wataweza kujiajiri wenyewe, kuanzisha biashara zao, na kuwa sehemu ya suluhisho la changamoto ya ajira nchini, ambapo vijana watakaonufaika watakuwa na fursa ya kupatiwa mikopo isiyo na dhamana kwa ajili ya kuendeleza biashara zao baada ya mafunzo.
Vilevile, Dkt. Madele amebainisha kuwa matokeo ya kuwepo kwa Mradi huo ni kutokana na uongozi madhubuti wa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi mahiri wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutambua kwa kina changamoto ya ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana, ndiyo maana Mheshimiwa Rais amechukua juhudi za makusudi kuhakikisha fedha hizo zinapatikana kwa ajili ya kuboresha maisha ya vijana kupitia miradi yenye tija kama huo wa BBT.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Ndg. Daudi Mayeji, amesema Mradi huo hautaishia kwa vijana waliopo Dodoma tu bali kwa vijana kutoka maeneo mbalimbali ya nchi, ambapo Mpango huo utamuwezesha kijana kuhudumia Mbuzi 100 kwa pamoja.
Pia, Ndg. Mayeji amesema Mradi huo unategemea ndani ya miaka mitano kutoa Mafunzo kwa vijana takriban 1750 na Serikali tayari imeshatenga eneo la hekta 2000 kwa ajili ya kupanda Malisho ya Mifugo.
Naye, Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, ambaye ni Afisa Tarafa ya Kongwa, Ndg. Jeremiah Kabebwa ameishukuru Wizara kwa kuwaletea Mradi wenye fursa kwa vijana ambapo ameihakikishia Wizara kuwa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya itahakikisha vijana wote wanaichangamkia fursa hiyo ili kuweza kujikwamua kiuchumi.