Baadhi ya wajumbe wa KU wilaya pamoja na wapiganaji wakiwa katika picha ya pamoja baada ya makabidhiano
Mkuu wa Zimamoto wilaya ya Bahi A/Insp Mussa Msengi akipokea funguo za mtambo wa Maokozi uliokabidhiwa wilaya ya Bahi mbele ya baadhi ya wajumbe wa KU wilaya kutoka kwa ASF P. Mwambene
Kaim DAS, Subiri Kajuni akipokea ufunguo kutoka kwa ASF Peter Mwambene kwaajili ya kuujaribu mtambo huo ili kudhibitisha upokeaji
…. .
*Jumamosi, 11 April 2026*
Kwa niaba ya Kamanda wa Mkoa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Dodoma, *ASF P. J. Mwambene* amekabidhi mtambo mpya wa Maokozi kwa Mkuu wa Zimamoto Wilaya ya Bahi, *A/Insp Mussa Msengi* ikiwa ni hatua ya kuimarisha uwezo wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika kukabiliana na majanga ikiwemo Maokozi ya ajali barabarani.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, *ASF Peter Mwambene* alieleza kuwa ujio wa mtambo huo utasaidia kutoa huduma zilizokusudiwa kwa ubora wa hali ya juu na wakati kwa wilaya ya Bahi na maeneo jirani ya wilaya ya Manyoni ambayo yako karibu sana na wilaya ya Bahi
*ASF P. J. Mwambene* Alisisitiza umuhimu wa kutumia vifaa hivyo kwa weledi na kuvitunza ili viweze kudumu na kuendelea kutoa huduma kwa jamii
Kwa upande wake, *A/Insp Mussa Msengi* alishukuru uongozi wa Mkoa chini ya kiongozi wake mahiri *SSF Rehema J Menda* kwa kuipatia Wilaya ya Bahi Mtambo huo, akiahidi kuutunza na kuutumia ipasavyo katika kuokoa maisha na mali za wananchi pamoja na kuimarisha juhudi za kinga na tahadhari dhidi ya majanga.
Katika mapokezi hayo Kamati ya Usalama wilaya, iliwakilishwa na baadhi ya wajumbe akiwemo Kaimu DAS, Subiri L. Kajuni, DBC Theopster Tembo, ASP Luka. J. Ketto kwa niaba ya OCD, Nasir Mwasema kwa niaba ya DSO pamoja na Kudra Kitabuge kutoka idara ya elimu Msingi, Halmashauri ya wilaya ya Bahi
Katika nasaha zao, Kaimu DAS, ameshukuru kwa upatikanaji wa Mtambo huu na kutanabaisha kuwa wilaya imepokea kwa furaha kubwa na ofisi ya DC itashirikiana na ofisi ya DFO kuutunza kwaajili ya kudumu kwa muda mrefu, kwani ni hatua kubwa ya usalama ambayo wilaya imepatiwa.
Kwa upande wake Mkuu wa TAKUKURU wilaya *Teopister Tembo* amesema ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa ujio wa mtambo huu kwani utaweza kuongeza kasi ya utendaji ndani ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kuwafikia wahitaji wa huduma za kidharura kwa uharaka zaidi wakati *Asp Luka J. Ketto* yeye pia alipongeza hatua hii ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kupatiwa kitendea kazi na kuona kuwa itakuwa ni faraja kwa wakazi na wapitaji wa Bahi kwa kuweza kufikiwa kwa urahisi wanapopata changamoto ikizingatiwa pia kuwa Bahi ina barabara kuu inayopitisha watu tofauti na vyombo vya usafiri ndani na nje ya nchi lakini pia maneno mengine ya shukrani yalitoka kwa *Bwn. Kudra Kitabuge* kutoka idara ya elimu msingi, Halmashauri ya wilaya ya Bahi ambapo yeye aliona mwanga sasa unaiangazia wilaya ya Bahi huku akizungumzia pia kwa upande wa wananchi na mali zao kuwa ni fursa kubwa kwao kupata mtambo huu ambao utawezesha huduma za maokozi kutolewa kwa uharaka na urahisi zaidi
Dhamira ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa sasa ni kuboresha Miundombinu na vifaa vya kisasa ili kuhakikisha usalama wa wananchi unaimarika kwa kiwango cha juu, hii ni hatua ya awali lakini Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kupitia Afande Kamishna Jenerali wa Zimamoto na Uokoaji *J. W. Masunga* limejipanga kuhakikisha Miundombinu zaidi ya kizimamoto inawekezwa ikiwemo ujenzi wa kituo chenye hadhi ya wilaya hapa wilayani, vitendea kazi vingine mbali mbali, nyongeza ya askari nk ili kuhakikisha kuwa usalama unakuwepo wakati wote.
Aidha baada ya mapokezi, DSO *Anastazia M. Sumawe* alipata pia fursa ya kuutembelea mtambo huo ambapo nae alipongeza serikali kwa hatua hii huku akimpongeza DFO sanjari na Kamanda wa Mkoa pamoja na Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kazi nzuri wanazoendela kupambana nazo.
Kwa ujumla wajumbe wote wameipongeza Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na *Dr. Samia Suluhu Hassan* , Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uwezeshaji mkubwa ambao amekuwa akiufanya kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na maeneo mengine
Mapokezi haya pia yametiliwa baraka na Mhe; Joacim Nyingo, Mkuu wa wilaya ya Bahi ambapo hakupata fursa ya kuhushuria kutokana na kuwa na majukumu mengine lakini ametoa baraka zote za mapokezi na kushukuru kwa ujio wa mtambo huu
Naambatisha baadhi ya picha za makabidhiano
ZMM 0468 FC AHMED OMARY
*CPR III DODOMA*


