RAIS DKT. SAMIA ATUNUKIWA SHAHADA YA UZAMIVU YA HESHIMA KUTOKA CHUO KIKUU CHA NASARAWA CHA NCHINI NIGERIA KWA NJIA YA MTANDAO.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akifuatilia hafla ya mahafali kwa njia ya mtandao ambapo ametunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Heshima

kutoka Chuo Kikuu cha Jimbo la Nasarawa, Keffi nchini Nigeria, tarehe 11 Aprili, 2026 Ikulu, Dodoma.

Mheshimiwa Rais ametunukiwa Shahada hiyo ya Uzamivu ya Heshima kwa kutambua mchango wake kama Kinara wa Nishati Safi ya Kupikia, Afya ya Mama na Mtoto, Taswira nzuri katika masuala ya Uongozi kwa Wanawake Afrika na Kusimamia Masuala ya Biashara hususani kwa Vijana Afrika.







 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza kwa njia ya mtandao na Chuo Kikuu cha Jimbo la Nasarawa, Keffi nchini Nigeria ambacho kimemtunuku Shahada ya Uzamivu ya Heshima , tarehe 11 Aprili, 2026 Ikulu, Dodoma.