Ulega atoa neno semina ya wabunifu majengo Moro

Na MWANDISHI WETU

WAZIRI  wa  Ujenzii, Abdalllah Ulega, amesema serikali itaendelea kushirikiana kikamilifu na wabunifu majengo kuhakikisha kuwa na miji iliyopangika vyema na manengo salama.

Aidha amewataka wabunifu majengo nchini kuwekeza taaluma yao katika ubunifu kwa kutumia teknolojia  kubwa lakini kwa gharama nafuu.

Ulega ameyasema hayo, mjini Morogoro, alipofungua semina ya siku mbili ya wabunifu majengo kuhusu  upangaji miji na ujenzi wa nyumba bora zinazo zingatia teknolojia ya sasa na zamani (AAT CPD)

Semina hiyo  iimeshirkishs  wataalamu zaidi ya 300 kutoka ndani na nje ya ncjhi imeandaliwa na Chama cha Wabunifu Majengo Tanzania (AAT)

Waziri Ulega amesema fani ya ubunifu majengo ni fani muhimu  hivyo kuwataks wataalamu hao kujitangaza ili jamii iwatambue na kuwatumia.

“Vilevile  nyie ni wanasayansi wazuri. Tumieni  ubunifu wenu kubuni  mambo ya teknolojia  kwa gharama nafuu  itakayo endana na mahitaji na mazingira ya nchi yetu” amesema Ulega.

Amebainisha katika dunia ya sasa wanasayansi wanatumia  teknolojia kubuni vitu  kwa gharama nafuu vinavyo weza kuingia katika ushindani na vitu vya teknojia ya gharama kubwa.

“Hivyo nasisitiza  mtumie ubunifu wenu katika kuisaidia jamii yetu kwa kutumia teknolojia ya gharama nafuu yenye tija,” amebainisha.

Pia ameitaka AAT kuitangaza taaluma hii kwani wabunifu majengo wakitumika vyema wanasaidia taifa kuwa na miji bora inayoendelea yenye ujenzi salama na iliyopangika.

“Fani yenu  ni muhimu lakini imefichwa. Huenda imefichwa zaidi  na wahandisi ambao wanafanya kazi zote za ujenzi. Mkijitangaza mkajulikana jamii itawatumia na itaachana pia na kuwatumia vishoka katika ujenzi,” ameeleza Waziri Ulega.

Amebainis  serikali chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, itaendelea kushirikiana na wabunifu majengo nchini kwa kuzifanyia marekebisho,sheria na kanuni mbalimbali ili kuketa uwajibikaji bora ma ufanisi.

Aidha ameipongeza  AAT kwa kuandaa semina hiyo  hasa kuwashirikisha wanafunzi wa vyuo na vyu vikuu wanasomea taaluma mbalimbali za kada hiyo ya ujenzi jambo alilosema litaleta tija kwa taifa.

Awali Rais  wa AAT  Mack  T’Chawi, alisema semina hiyo itasaidia kutoa elimu ya namna ya kupanga miji inayobadilika kullngana na teknolojia ya sasa na ya zamani.

Katibu  Mtendaji wa AAT Attie  Ally, alisema katika kuunga mkono jitihada  za Rais Dk. Samia kukiza sekta ya utalii nchini washiriku wa semina hiyo leo watakwenda kutalii katika Mbuga ya Wanyama ya Mikumi mkoani humo.

“AAT tunaujga mkono jitihada za Rais Dk. Samia za kutangaza utalii, hivyo washiriki wote wa semina hii ya kimataifa tutawapeleka  Mikumi kutalii,” almesema  Attie.

Washiriki wa semina hiyo wamesema ina tija kubwa kwao katika kubadilishana uzoefu hasa kipindi hiki ambapo miji mingi inaendelea kukua kutokana na ongezeko la watu.