Bilo, Ruangwa hatihati kushuka WPL

TIMU mbili zilizopanda daraja msimu huu katika Ligi ya Wanawake, Ruangwa Queens na Bilo FC, ziko kwenye hatari ya kushuka daraja kutokana na mwenendo wao msimu huu.

Timu hizo ambazo zilipanda kutoka ligi ya mikoa zimejikuta zikishika nafasi za chini kwenye msimamo, Ruangwa Queens ikiwa nafasi ya 11 na Bilo FC ya 12.

Ruangwa Queens imeshinda mchezo mmoja pekee, sare moja na kupoteza 11, ikiwa na pointi nne na tofauti ya mabao 22, hali inayoonyesha changamoto kubwa ya kukabiliana na kasi na uzoefu wa ligi kuu.

Kwa upande wa Bilo FC hali ni ngumu zaidi, kwani nao imeshinda mechi mmoja na sare moja pekee, ikipoteza 11 na ina pointi nne.

Timu zote zimekuwa na muendelezo mbaya wa ligi jambo linaloonyesha kuwa huenda zikarudi zilipotoka kama hazitapambana kwenye meci zilizosalia.

Changamoto kubwa kwa timu zote mbili ni wameshindwa kuendana na kasi ya ushindani, uzoefu mdogo wa wachezaji wengi kwenye ligi, pamoja na tofauti ya maandalizi ikilinganishwa na timu zilizokaa muda mrefu kwenye ligi hiyo.

Zimesalia mechi tisa kumaliza ligi lakini katika mechi hizo Bilo na Ruangwa bado ina nafasi ya kufanya kitu na kusalia kwenye ligi.