Global Publishers
April 13, 2026
0 Comments
Klabu ya Mamelodi Sundowns imepiga hatua kubwa kuelekea fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 1-0 dhidi ya Espérance Sportive de Tunis katika mchezo wa nusu fainali uliopigwa nchini Tunisia.
Katika dimba la Stade Olympique Hammadi Agrebi, Sundowns walionyesha ubora wao kwa kupata bao pekee la ushindi dakika ya 52 kupitia mshambuliaji Brayan Leon.
Hata hivyo, mchezo huo haukukosa drama baada ya beki Grant Kekana kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 84, jambo lililowaacha Sundowns wakimaliza mechi wakiwa pungufu ya mchezaji mmoja.
Ushindi huo wa ugenini unaipa Sundowns faida muhimu ya bao moja kabla ya mechi ya marudiano itakayochezwa Aprili 18, 2026 nchini Afrika Kusini.
Matokeo kwa sasa:
Sundowns 1-0 Esperance (jumla)
Kwa upande mwingine wa nusu fainali:
RS Berkane wanakutana na AS FAR Rabat huku FAR Rabat wakiwa mbele kwa jumla ya mabao 2-0.
Nani Atafika Fainali?
Sundowns sasa wanahitaji sare tu au ushindi wowote ili kukata tiketi ya fainali, wakati Esperance wanalazimika kushinda kwa zaidi ya bao moja ili kurejea kwenye ushindani.
Mashabiki wa soka barani Afrika wanasubiri kwa hamu kuona kama Sundowns watafanikiwa kukamilisha kazi nyumbani au Esperance watafanya “comeback” ya kushtua.