Radi yaua wanafunzi watatu Shule ya Msingi Msongola Dar
Dar es Salaam. Wanafunzi watatu wa Shule ya Msingi Msongola, iliyopo Kivule wilayani Ilala jijini Dar es Salaam, wamefariki dunia kutokana na kupigwa na radi. Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amethibitisha tukio hilo na amesema tukio hilo limetokea leo Jumatano Machi 18, 2026. “Ni kweli wanafunzi wetu…