Mkurugenzi huduma za wakunga ataja mikakati ya kuokoa maisha ya wajawazito
Dar es Salaam. Wakati dunia ikiendelea kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani Machi 8 ya kila mwaka, mjadala kuhusu haki, afya na ustawi wa wanawake unapewa uzito katika sekta mbalimbali, ikiwamo ya afya ya uzazi. Kwa Tanzania, moja ya maeneo yanayopewa kipaumbele katika kulinda maisha ya wanawake ni kupunguza vifo vinavyotokana na ujauzito na uzazi. Lengo…