Safari ya mjamzito aliyebebwa kwa machela kwenda kujifungua aeleza maumivu, ushujaa na furaha
Kilolo. Nadhani tunakumbuka picha ya mama mjamzito kutoka Kiwalamo, wilayani Kilolo, aliyebebwa kwa machela na wanakijiji akiwa katika uchungu wa kujifungua kutokana na barabara mbovu hadi Hospitali ya Dabaga kwenda kujifungua. Hii ni simulizi ya kishujaa ya Zaineth Kipingi, mama wa Moreen, aliyejifungua kwa mara ya kwanza Juni mwaka huu akibebwa kwenye machela kutoka Kiwalamo…