Sh500 milioni kupunguza changamoto ya maji Kimochi
Moshi. Naibu Waziri wa Maji, Kundo Mathew, amesema Serikali itapunguza kwa kiasi kikubwa changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa zaidi ya wananchi 16,000 wa Kata ya Kimochi, Wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro ndani ya siku 90. Akizungumza jana Jumatano, Februari 25, 2026, wakati akisikiliza kero za wananchi wa eneo hilo, Kundo alisema…