Shahidi aieleza Mahakama chanzo jengo la CCM kuchomwa moto
Dar es Salaam. Mkaguzi wa Polisi mwenye namba PF 20122, Jafari Nguli (49) ameieleza Mahakama jinsi alivyobaini chanzo cha moto uliyounguza na kuteketeza jengo la Chama cha Mapinduzi (CCM) Kivule, lililopo Kata ya Majohe, Wilaya ya Ilala. Nguli ambaye alikuwa mpelelezi mkuu katika kesi hiyo, amedai upelelezi wake ulibaini chanzo cha kuchoma jengo hilo kilitokana…