Prisons yaachana na Otieno, Nsajigwa atajwa kumrithi

BAADA ya Tanzania Prisons kufikia makubaliano ya pande mbili kuachana na Kocha Zedeckia Evans Otieno, inaelezwa iko katika hatua nzuri ya mikoba yake kumkabidhi Shadrack Nsajigwa ‘Fuso’ kutoka kwa maafande wa Transit Camp. Taarifa ya Tanzania Prisons kuachana na Otieno iliyotolewa leo Februari 25, 2026 na Afisa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, ‎Godfrey Madegwa, imesema:…

Read More

Mbunge Kabati awarejeshea tabasamu wenye ulemavu 13

Iringa. Furaha na shangwe zimetawala katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa, baada ya watu 13 wenye ulemavu kukabidhiwa viungo bandia vya miguu vilivyogharimiwa na Mbunge wa Kilolo, Ritta Kabati kupitia Taasisi ya Ritta Kabati Trust Fund. Wanufaika hao wamesema kwa muda mrefu walikwamishwa na gharama kubwa za viungo saidizi, hali iliyowafanya waendelee kuishi…

Read More

Mvua zakwamisha ujenzi wa barabara, mbunge ang’aka

Tunduru. Ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilomita 1.7 katika Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, mkoani Ruvuma, umeshindwa kukamilika kwa wakati kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika eneo hilo. Barabara zinazojengwa kwa kiwango cha lami ni kipande cha Boma–Mkwanda chenye urefu wa mita 700 na Mlingotini–Supermarket chenye urefu wa kilomita 1. Akizungumza mbele ya Mbunge…

Read More

Tathmini yabaini udhaifu wa kuhesabu kwa wanafunzi wa awali

Dodoma. Tathmini iliyofanywa na Serikali kuhusu stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa wanafunzi wa darasa la awali hadi la tatu imebaini kuwa stadi ya kuhesabu iko chini ikilinganishwa na stadi za kusoma na kuandika. Kwa mujibu wa matokeo ya tathmini hiyo, wanafunzi wengi wanafanya vizuri zaidi katika kusoma, ikifuatiwa na kuandika, huku kuhesabu…

Read More

Sababu Rita kuvunja Bodi ya Wadhamini Kanisa la Wasabato

Dar es Salaam. Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita) umeivunja Bodi ya Wadhamini ya Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA) Tanzania, kufuatia tuhuma za ubadhirifu wa mali za kanisa na kushindwa kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria. Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Februari 25, 2026 jijini Dar es Salaam, Mtendaji Mkuu wa…

Read More

Wasiwasi ulioibuka kuhusu kuwarejesha nyumbani wakimbizi wa Burundi kutoka Tanzania ‘kwa kutumia nguvu’ — Global Issues

Hadi kufikia mwishoni mwa Novemba 2025, kulikuwa na zaidi ya wakimbizi 140,000 wa Burundi katika nchi jirani ya Tanzania, ambao wamekimbia machafuko ya wenyewe kwa wenyewe kwa miaka mingi nchini Burundi. Wakati maelfu wanaendelea “kurejeshwa kwa hiari”, afisa wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) anasema maelfu bado wanaweza kuhitaji ulinzi wa…

Read More

Nida kubadili muundo vitambulisho vya Taifa

Dar es Salaam. Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) iko mbioni kuanza kutoa aina mpya ya Vitambulisho vya Taifa ambavyo vimeboreshwa na kuongezewa huduma nane ndani yake. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Vitambulisho wa Nida, Edson Guyai katika mahojiano maalumu na Mwananchi yaliyofanyika Jumatatu, Februari 23, 2026. Wanufaika wa vitambulisho hivi vipya watakuwa…

Read More