DC KIBITI ABANA VIKUNDI CHECHEFU, AAGIZA MAJINA YAWASILISHWE HARAKA
MKUU wa Wilaya ya Kibiti, Kanali Joseph Kolombo ameitaka Idara ya Maendeleo ya Jamii kuwasilisha majina ya vikundi vyote ambavyo havijarejesha mikopo ya asilimia 10, maarufu kama ‘chechefu’ vinavyokwamisha juhudi za maendeleo. Kanali Kolombo alitoa agizo hilo Machi 17, 2026, wakati wa hafla ya utoaji wa mikopo kwa vikundi 20 kati ya 101 vilivyokidhi vigezo,…