MAELEKEZO YA MRAJIS KWA VYAMA VYA USHIRIKA KUTUMIA MIZANI ZA KIDIGITALI KATIKA UPIMAJI WA MAZAO
Mrajis wa Vyama vya Ushirika, Dkt. Benson Ndiege amevitaka Vyama vya Ushirika vya Mazao nchini kutumia mizani za kidigitali katika kupima mazao ya wakulima ili kuondoa udanganyifu na kumlinda mkulima. Mrajis ametoa maelekezo hayo kupitia barua ya tarehe 13 Machi, 2026 aliyowaandikia Wenyeviti na Wajumbe wa Bodi wa Vyama vya Ushirika vya mazao Tanzania Bara…