Tume yabaini changamoto lukuki mfumo wa kodi, yasisitiza mageuzi
Dar es Salaam. Baada ya takribani miaka 30 tangu kufanyika kwa mapitio makubwa ya mfumo wa kodi nchini, Tume ya Rais ya Kutathmini Maboresho ya Mfumo wa Kodi imebaini changamoto lukuki zinazoathiri walipa kodi na mazingira ya uwekezaji, huku ikisisitiza umuhimu wa mageuzi ya haraka ili kufikia malengo ya maendeleo ya muda mrefu. Julai 31,…