Ofisa wa Polisi jela miaka miwili kwa mauaji
Iringa. Mahakama Kuu Kanda ya Iringa imemhukumu askari wa Jeshi la Polisi, Sajenti Rogers Mmari (F.4987) wa Kituo cha Polisi Ipogolo, kwenda jela kwa miaka miwili baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kuua bila kukusudia. Tukio hilo lilitokea Desemba 14, 2024 Mtaa wa Ipogolo, Manispaa ya Iringa ambapo Mshtakiwa huyo alimpiga marehemu Nashoni Kiyeyeu…