Dk Tulia agusa wahitaji 204, misikiti 17 wagawiwa futari, masheikh watoa neno
Mbeya. Mbunge wa Uyole mkoani hapa, Dk Tulia Ackson, amerejesha kicheko kwa waumini 204 wa dini ya Kiislamu, wakiwemo wazee waishio katika mazingira magumu, kwa kutoa futari katika misikiti 17 iliyopo katika kata 13 jimboni kwake. Hatua hiyo ni sehemu ya sadaka katika kuhitimisha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani na kuelekea kuungana na Watanzania…