Azam FC Yaendeleza Ubabe Dhidi ya Simba, Yadumisha Rekodi ya Kutopoteza

Global Publishers
April 5, 2026
0 Comments

Klabu ya Azam FC Aprili 5, 2026 imeendelea kuonesha ubora wake msimu huu baada ya kutoka sare ya bila kufungana dhidi ya Simba SC katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Azam Complex.

Matokeo hayo yanaifanya Azam FC kuendeleza rekodi yao ya kutopoteza (unbeaten) msimu huu, huku ikiwa ni mara ya pili kuwazuia Simba SC kupata ushindi baada ya awali kuwafunga katika mchezo wa mzunguko wa kwanza.

Kwa upande wa Simba, sare hiyo inaendelea kuwaumiza katika mbio za ubingwa, wakisalia nafasi ya pili wakiwa na alama 35 baada ya michezo 16, huku Azam FC (Wanalambalamba) wakishika nafasi ya tatu kwa alama 33 baada ya michezo 17.

Licha ya juhudi za timu zote mbili kutafuta ushindi, safu za ulinzi zilikuwa imara, na kufanya mchezo huo kumalizika bila mshindi.

Matokeo haya yanaongeza presha katika mbio za juu ya msimamo wa ligi, huku Azam FC ikiendelea kuwa mwiba kwa vigogo na kudhihirisha kuwa ni moja ya timu hatari msimu huu.