TCCA YAMPONGEZA DKT. NASRA KUSAIDIA SEKTA YA ANGA

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania TCAA kupititiakwa mkurugenzi wake Ramadhani Msangi imempongeza Mkurugenzi wa kituo cha afya cha Aerospace Medical and Training Centre (AMTc) Kwa kutengeneza kitabu chenye muongozo wa kutoa huduma za afya kwenye ndege, akisema huo ni mwanzo mpya wa kusaidia huduma za anga nchini Tanzania.

Wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho jijini Dar es Salaam, Dkt. Nasra Nassor Omar amesema hiyo ilikuwa ni ndoto yake siku nyingi kusaidia sekta ya anga nchini.

Baadhi ya watu walio katika sekta hiyo wakiwemo Annamaria Rogatus Nzamba, Ramla Mshana na Lilian Felix Mlolere nao wametoa uzoefu wao kwa sekta hiyo.