Nafasi 14 Zatangazwa Maswa, Mwisho wa Maombi Aprili 13

Global Publishers
April 6, 2026
0 Comments

Halmashauri ya Wilaya ya Maswa imetangaza nafasi 14 za ajira kwa Watanzania wenye sifa, kufuatia kibali kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Kwa mujibu wa tangazo hilo lililotolewa Machi 31, 2026, nafasi hizo zinahusisha kada ya madereva pamoja na waandishi waendesha ofisi.

Nafasi Zilizotangazwa:

1. Dereva Daraja la II – Nafasi 10
Waombaji wanatakiwa kuwa na elimu ya Kidato cha Nne, leseni ya daraja C au E, pamoja na uzoefu wa kuendesha gari kwa angalau mwaka mmoja bila kusababisha ajali. Aidha, ni lazima wawe wamepata mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari kutoka vyuo vinavyotambuliwa kama VETA.

 2. Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II – Nafasi 4

Kwa upande wa nafasi hizi, waombaji wanapaswa kuwa na elimu ya Kidato cha Nne au Sita, cheti cha NTA Level 6 au mafunzo ya uhazili. Pia wanatakiwa kuwa na uwezo wa kuchapa kwa kasi ya maneno 120 kwa dakika pamoja na ujuzi wa matumizi ya kompyuta.

Masharti Muhimu kwa Waombaji:

  • Awe raia wa Tanzania mwenye umri kati ya miaka 18 hadi 45
  • Awe ameambatanisha vyeti halali vilivyothibitishwa
  • Awe na wasifu binafsi (CV) pamoja na wadhamini watatu
  • Waombaji waliostaafu au walioajiriwa serikalini hawaruhusiwi kuomba

Mwisho wa Kutuma Maombi Aprili 13, 2026

Jinsi ya Kutuma Maombi:

Barua ya maombi ielekezwe kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa.