WAZIRI MKUU DKT MWIGULU AKAGUA ATHARI ZA MOTO SIMU 2000.

……….

Waziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mwigulu Nchemba leo April 6, 2026 amefika Simu 2000 Wilaya ya Ubungo kukagua madhara ya moto ambao umeteketeza vibanda vya wafanyabiashara wadogo takribani 580.

Waziri Mkuu akiongea na wafanyabiashara waliopata athari katika eneo la simu 2000 ametoa pole kwa waathirika wote ambapo amesema “Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan anawapeni pole na ameagiza uchunguzi wa kina ufanyike haraka.

Aidha Mhe Mwigulu Nchemba amesema hoja zote zilizotolewa amezipokea na akaelekeza yafuatayo yafanyike kwa haraka ikiwemo kusafisha eneo lililoungua kwa moto hadi kesho liwe tayari ili kama kunamfanyabiashara anaweza kufanya biashara aweze kufanya, pia ameagiza uwepo wa stendi Simu 2000 ambapo amemuagiza Katibu Mkuu pamoja na Mkuu wa Mkoa kukutana na wadau wote kupitia disign ya eneo hilo na kuhakikisha linakidhi mahitaji yote muhimu.

Vilevile amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Ubungo kusimamia na kuhakisha dosari za waliokuwa wakiuza bidha na wamiliki wa vibanda kufahamika ili haki itendeke kwa sababu viko viashiria vya mtu kumiliki kibanda na kumkodisha mwingine ambaye ndiye anafanya biashara.

Sanjari na hilo Waziri Mkuu ameagiza wahanga wa moto sokoni hapo kupatiwa mikopo na Halmashauri ya Ubungo pasipo kuwa na mashariti magumu pia anatambua kuwa wapo waliokopa kwenye taasisi za kifedha hivyo ameagizi kufanya mazungumzo na taasisi hizo ili wafanya biashara wapewe muda kidogo wa kurejesha.

Suala la Masoko kwenye Kata mbili za wilaya ya Ubungo Mhe Mwigulu amesema litatekelezwa kwa kuwa Mhe Rais alishatoa maelekezo.

Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa Mhe Albert Chalamila amemshukuru waziri Mkuu kwa utendaji wake wa kazi bila kujali sikukuu amekuja na kuwatakia hali wahanga wa moto hivyo anamshuru sana. Vilevile RC Chalamila ametoa ufafanuzi wa taaruki mbalimbali zilizotokea katika Mkoa ikiwemo suala la kupanda kwa mafuta ya magari, watu kupoteza nyeti zao jambo ambalo sio sahihi pamoja na janga la moto katika Soko la Simu 2000.

Mwisho Mhe Mwigulu Nchemba ameagiza suala la amani ni wajibu wa kila mtu kuhakikisha anakuwa sehemu ya kulinda amani pale anapoona viashiria vya aina yoyote atoe taarifa kwa mamlaka husika.