Epuka Makosa Haya 9 Unaponunua Blueberries

Global Publishers
April 7, 2026
0 Comments

Matunda ya blueberries ni miongoni mwa vyakula vinavyopendwa sana wakati wa msimu wa joto, si tu kwa ladha yake tamu bali pia kwa faida zake kiafya kama kusaidia kumbukumbu, kupunguza shinikizo la damu na kuwa na kiwango kidogo cha kalori.

Hata hivyo, wataalamu wa lishe wanaonya kuwa watu wengi hufanya makosa wanaponunua matunda haya, jambo linaloweza kuwafanya wapate blueberries zisizo fresh au zisizo na ladha nzuri.

1. Kudhani kubwa ndiyo bora
Blueberries kubwa si lazima ziwe tamu zaidi. Mara nyingi ndogo huwa na ladha kali na tamu zaidi.

2. Kununua zenye unyevunyevu au maji chini ya kopo
Maji au juisi chini ya kifungashio ni dalili kuwa matunda yameanza kuharibika.

3. Kufikiri yataiva zaidi nyumbani
Tofauti na ndizi au parachichi, blueberries haziendelei kuiva baada ya kuvunwa.

4. Kutoangalia ukungu (mold)
Hakikisha unachunguza hasa chini ya kifungashio kwani zinaweza kuwa tayari zimeanza kuoza.

5. Kuchagua zilizosinyaa (wrinkled)
Hizi huashiria kuwa zimepoteza unyevu na si fresh tena.

6. Kuvutiwa na zilizo shiny sana
Blueberries fresh huwa na mwonekano wa vumbi laini (dusty). Zikiwa shiny sana huenda ni za zamani.

7. Kununua kwenye vifungashio visivyo na hewa
Kifungashio chenye matundu husaidia kudumisha ubora wa matunda kwa kuruhusu hewa kupita.

8. Kupuuza harufu
Zikiwa na harufu ya uchachu au uvundo, usizinunue. Blueberries nzuri huwa na harufu nyepesi na safi.

9. Kudhani lazima ununue organic pekee
Ingawa organic zinaweza kuwa bora kidogo, hata zisizo organic bado ni salama na zina virutubisho sawa.