Global Publishers
April 7, 2026
0 Comments
Rais Samia Suluhu Hassan leo ameshiriki Dua maalum ya kumuombea aliyekuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Hayati Abeid Amani Karume ikiwa ni miaka 54 tangu kuuawa kwake.
Dua hiyo pia imehudhuriwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Waziri Mkuu wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba.
Baada ya Dua hiyo maalum iliyofanyika Afisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kisiwandui, Zanzibar leo Aprili 7, 2026, Rais Samia, Rais Mwinyi na viongozi wengine, waliweka mashada ya maua kwenye kaburi la Hayati Karume.





