Okello Atengeneza Historia! Assist 3, Yanga Yaisambaratisha Pamba 3-0

Global Publishers
April 8, 2026
0 Comments

Klabu ya Yanga imeonyesha ubabe mkubwa baada ya kuichapa Pamba Jiji FC mabao 3-0 katika dimba la CCM Kirumba Stadium, Mwanza, kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Nyota wa mchezo alikuwa Allan Okello aliyetoa assist tatu safi (hat-trick of assists), akiongoza ushindi huo mkubwa wa Yanga.

Mshambuliaji Mudathir Yahya alifungua pazia dakika ya 8 kwa pasi ya Okello, kabla ya kurudi tena dakika ya 35 kufunga bao la pili tena kwa assist ya nyota huyo huyo.

Baada ya presha kubwa, Maxi Nzengeli alihitimisha karamu ya mabao dakika ya 68 kwa bao la tatu, likiwa pia limetengenezwa na Okello.

Matokeo Kamili:
Pamba Jiji FC 0-3 Yanga SC
⚽ 08’ Mudathir (🅰️ Okello)
⚽ 35’ Mudathir (🅰️ Okello)
⚽ 68’ Maxi (🅰️ Okello)