Na Diana Byera, Bukoba
WIZARA ya Katiba na Sheria imeanza kutoa mafunzo kwa wajumbe wa bodi za usuluhishi wa migogoro ya ndoa, kutokana na ongezeko la kesi za talaka nchini,
Akifungua mafunzo hayo Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Katiba na Sheria Franklin Rwezimula amesema mafunzo hayo yameanzia mkoani Kagera kwa lengo la kuongeza weledi na mbinu mpya za usuluhishi wa ndoa katika jamii ili kujenga familia bora na jamii yenye mshikamano
“Takwimu zinaonyesha talaka zilizosajiliwa mwaka 2023 zilikuwa 711, mwaka 2024 zikapanda hadi 1,569, na mwaka 2025 talaka zilizosajiliwa zilikuwa 1,172 na hizo ni zile talaka tu zilitoleawa taarifa na ndoa nyingine zimekuwa zikivunjika kimya kimya bila kutolewa taaarifa na kuhatarisha ustawi wa familia na jamii kwa ujumla.”
Amefafanua bodi za usuluhishi zinapaswa kufanya kazi kwa weledi na kujiepusha kuwa mahakimu huku akidai bodi hizo zisiwe sehemu ya kupokea rushwa Bali zijikite kuondomitafaruku kutovujisha Siri na Kutenda haki.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Sheria kwa umma Obadia Kamea amesema uwepo wa wajumbe wa bodi ya usuluhishi Kwa ngazi ya kata nchi nzima unalenga kupunguza Mrundikano wa kesi za talaka zinazoenda mahakamani
Amesema pia mafunzo haya yanalenga kuimarisha mbinu mpya , usuluhishi kulingana na hali ya kisasa ya malalamiko makubwa ya ndoa na migogoro iliyopo kwa sasa ukilinganisha na miaka ya Zamani .
Awali Issaya Tendega ambaye ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Kagera amesema migogoro ya ndoa isipotatuliwa kwa wa wakati inasababisha ofisi za viongozi ngazi ya wilaya na mikoa kuwa na mrundikano wa kesi ambo ambalo linasababisha viongozi kutumia muda mrefu Kufanya usuluhishi kuliko kufanya kazi Nyingine.
“Ofisi za wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa wanapokea kesi nyingi za ndoa na zinatumia muda mrefu sana ,tunaamini wajumbe wa haya mabaraza wakifanya kazi yao vizuri migogoro ya ndoa itapungua ,tunaomba baada ya mafunzo haya mfaye kazi kwa weledi ili kupunguza kesi nyingi za ndoa mahakamani na ofisi za viongozi”alisema Tendega
Awali Jawadu Mwanandege ambaye ni Mjumbe wa bodi ya usuhishi wa ndoa ameishukuru Serikali kwa namna inavyoendela kuimarisha mafunzo na mbinu za utatuzi kwa ngazi ya mabaraza ambapo alisema kuwa Mafunzo hayo yatawajengea uwezo wa kufanya usuluhishi na kufanya kazi kwa haki.
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
