SINGIDA Black Stars imemalizana na kocha Papi Kimoto anayetua kuifundisha timu hiyo ambayo hivi karibuni ilitangaza kuvunja benchi lote la ufundi.
Kimoto, raia wa DR Congo anatua Singida BS baada kuachana na Union Maniema iliyoishia hatua ya 16 bora katka Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu.
Taarifa kutoka nchini DR Congo ni kwamba, juzi usiku Singida ilimtumia mkataba Kimoto na jana asubuhi pande hizo mbili zikakubaliana kuingia ndoa mpya.
Kimoto anatua Singida kuwa kocha mkuu baada ya timu hiyo kuvunja benchi la ufundi lililokuwa likiongozwa na kocha mkuu, Mkenya, David Ouma na Meneja Mkuu, Othman Najjer raia wa Tunisia, uamuzi uliochukuliwa kutokana na kile kilichoelezwa ni matokeo mabaya.
Awali Singida ilikuwa imchukue kocha Guy Bukasa anayeifundisha timu ya taifa ya vijana ya DR Congo lakini jamaa akagoma kuachana na majukumu yake mpaka mkataba wake utakapomalizika.
Utata mwingine kwenye kumchukua Bukasa ilikuwa ni juu ya makubaliano ya muundo wa benchi lake la ufundi akitaka kuja na wasaidizi wake wote wa kiufundi.
Kimoto amekubali ajira hiyo akija na wasaidizi wawili kwenye benchi jipya la timu hiyo ambapo wakati wowote wiki hii a tatua Tanzania kuanza kazi.
“Kimoto amemalizana na Singida ndiye anakuja huko kuifundisha timu hiyo, amesaini mkataba leo (jana), atakuja huko Tanzania ndani ya wiki hii,” alisema mmoja wa wasimamizi wa kocha huyo.
“Singida ilikuwa inataka kocha sasa hivi baada ya kufuta benchi lake, Bukasa ilikuwa ngumu hakutaka kuondoka vibaya pale DR Congo ndio maana wakaweka nguvu kwa Kimoto.
