Global Publishers
April 9, 2026
0 Comments
Simba leo Aprili 9, 2026 ameshindwa kupata ushindi kwa mara ya kwanza dhidi ya TRA United baada ya kulazimishwa sare tasa (0-0) katika dimba la Sheikh Amri Abeid, Arusha. Ni matokeo ambayo yanaongeza presha kwenye mbio za ubingwa kwa upande wao.
Simba sasa wanaendelea kushikilia nafasi ya pili wakiwa alama 8 nyuma ya vinara Young Africans SC, ambao wana alama 36 baada ya kucheza mechi 17 (na mechi moja pungufu). Hii inaifanya mbio za ubingwa kuwa ngumu zaidi kwa Simba, ambapo kila mchezo unaobaki unakuwa muhimu sana.

Katika mchezo huo huo, Simba walimaliza pungufu baada ya mchezaji Nouma kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 87’, jambo lililoathiri mipango yao ya kusaka ushindi wa mwisho.
Kwingineko, Azam FC nao walilazimishwa sare tasa dhidi ya Mbeya City FC katika dimba la Tanzanite Kwaraa, Babati Manyara. Matokeo hayo yanawaacha wote wakigawana pointi moja kila mmoja.
📊 FT Results:
- TRA United 0-0 Simba SC 🟥 (Nouma 87’)
- Mbeya City 0-0 Azam FC