WATANZANIA WAOMBWA KUCHANGIA UJENZI JENGO LA MATIBABU YA MOYO-KCMC

Na Said Mwishehe,Michuzi TV

UONGOZI wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kilimanjaro Christian Medical Centre(KCMC) umewaomba Watanzania waliopo ndani na nje ya nchi kuchangia ujenzi wa jengo la matibabu ya moyo-KCMC ambapo kiasi cha Sh.bilioni 25 kinahitajika kukamilisha jengo hilo.

Akizungumza leo Aprili 9,2026 jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa KCMC Profesaa Gileard Masenga amesema ujenzi wa jengo hilo utagharimu Sh.bilioni 25 za kitandania na Vifaa tiba na vifaa vya hospitali vitagharimu jumla ya kiasi cha shilingi bilioni 25.

Aidha amesema amesema wataalamu watakaohudumia kitengo hicho tayari wameshapata mafunzo yao nchini India na Tanzania na wamepata ufadhiliwa kutoka kwa mdau aitwae Global Heartcare Foundation.

“KCMC tayari imeingia makubaliano ya ushirikiano na wadau wa kimataifa ambao wamekubali kufadhili asilimia 90 ya gharama za ujenzi.Hivyo tumekuja kwenu Watanzania kuomba mchangie asilimia 10 ya mchango wa ujenzi kwani tayari asilimia 90 ya fedha ya ujenzi ilishapatikana.”

Hivyo ametoa rai kwa watanzania wote (ndani na nje ya nchi) kuungana katika juhudi hiyo ya kitaifa kwani lengo ifikapo Julai mwaka 2027 huduma za matibabu ya moyo yawe yameanza kutolewa kuokoa maisha ya Watanzania wanaosumbuliwa na magonjwa ya moyo nchini.

“Huu si mradi wa KCMC pekee. Huu ni mradi wa Watanzania wote. Ni mradi wa kulinda maisha ya ndugu zetu, wazazi wetu, watoto wetu, na vizazi vijavyo.

“Tunawaomba Watanzania wa kila rika na kila nafasi vijana, wazee, wafanyabiashara, wafanyakazi, wakulima, viongozi, na diaspora yetu kuchangia kwa moyo wa uzalendo na mshikamano.Kila mchango ni muhimu. Kila mchango ni uhai. Kila mchango ni tumaini.”

Amesisitiza “Kwa pamoja, tunaweza kujenga kituo hiki.Kwa pamoja, tunaweza kuokoa maisha.Na kwa pamoja, tunaweza kuandika historia mpya ya huduma za afya chini Tanzania.”

Jinsi ya kuchagia Profesa Masenga amesema Watanzania wanaweza kuchangia kupitia njia zifuatazo: AKAUNTI JINA: KCMC MOYO

Bank of Africa – 04563580007

CRDB Bank – 0150686858800

NMB Bank – 40310194610

NBC Bank – 017172000770

MITANDAO YA SIMU:

Mixx by Yas – 15175376

Halotel (Halopesa) – 23758475

Aidha, kwa wale watakaopenda kutoa michango yao ana kwa ana, wanakaribishiwa kufika moja kwa moja katika hospitali ya KCMC huku akisisitiza kuwa jukumu la afya sio la Serikali tu. “Hiyo ndo maana KCMC inataka kuanza huduma hii.”

Amesema pia jengo hilo litakapokamilika litakuwa la kisasa lenye ghorofa tatu ambapo litakalojumuisha vyumba viwili vya upasuaji wa moyo (cardiac surgery theatre),maabara mbili za uchunguzi wa mishipa ya moyo (catheterization laboratory).

Pia vyumba vya wagonjwa mahututi (Intensive Care Unit – ICU) kwa watu wazima na watoto, Vitengo vya uangalizi maalum baada ya ICU (step-down ICU units),Vitanda 102 vya wagonjwa wa ndani,kliniki za wagonjwa wa nje, kitengo cha urekebishaji wa afya ya moyo (cardiac rehabilitation unit) na mabaara za uchunguzi na huduma za dawa.

Awali Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Watoto katika hospitali ya KCMC Dk.Ronald Mbwasi amesema kwa magonjwa ya moyo yasiyoambukiza kwa sasa yanachangia takribani asilimia 70 ya vifo duniani. Miongoni mwa magonjwa haya, magonjwa ya moyo na mishipa (cardiovascular diseases – CVDs) ndiyo chanzo kikuu cha vifo.

“Magonjwa kama Kiharusi (stroke) na Ugonjwa wa kuziba kwa mishipa ya moyo (ischemic heart disease) yanachangia sehemu kubwa ya vifo hivi. Zaidi ya asilimia 78 ya vifo vinavyotokana na magonjwa yasiyoambukiza hutokea katika nchi zenye kipato cha chini na cha kati (lower and middle income). 

“Magonjwa ya moyo ni miongoni mwa sababu kuu za wagonjwa kulazwa KCMC; takwimu za

hospitali zinaonyesha asilimia 14.4 ya wagonjwa wanaolazwa ni wagonjwa wa moyo ambapo hulazwa hospitalini kwa wastani wa siku 9 hadi 10…

“Na asilimia 38.5 ya wagonjwa wanaoruhusia hulazwa tena hospitalini baada ya muda na hivyo kiwango cha vifo kwa wagonj wa wa moyo ni takribani asilimia 18.3 ya vifo vyote vinavyotokea KCMC.”