DAR ES SALAAM KUPOKEA MWENGE WA UHURU APRIL 13, 2026

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila amewataka wananchi wa Mkoa huo kujitokeza katika mbio za Mwenge wa Uhuru unaotarajia kuwasili jijini humo aprili 13 mwaka huu ukitokea Mkoa wa Kaskazini Unguja ambapo utakimbizwa umbali wa kilometa 392.22 kwenye Wilaya zote tano za mkoa huo ukikagua, kuzimdua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi 35 yenye thamani ya shilingi bilioni 113.5

Akizungumza na waandishi wa habari RC Chalamila amesema shabaha ya mbio za mwenge wa uhuru ni kuleta umoja, mshikamano na udugu baina ya watanzania ambapo amesema aprili 13 baada ya kuwasili utakimbizwa wilayani Ilala, April 14 wilaya ya Kigamboni, April 15 wilaya ya Temeke, April 16 wilaya ya Ubungo na April 17 wilaya ya Kinondoni na April 18 Mkoa utakabidhi Mkoa wa Pwani.

RC Chalamila amesema Mwenge wa Uhuru kwa mwaka huu wa 2026 umebeba ujumbe wa kudumisha amani, umoja na mshikamano wa kitaifa chini ya kauli mbiu isemayo “Tanzania ni Yetu Sote, Tushikamane kwa Pamoja Kuleta Maendeleo”

Sanjari na ujumbe wa kudumu wa mbio hizo ambao ni kuimarisha mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI, Dawa za Kulevya Lishe, na Rushwa, hivyo ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika Wilaya zote ambako Mwenge wa Uhuru utakimbizwa.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh Albert Chalamila amezungumzia suala la Nishati ya mafuta ya petroli na diseli ambapo amewatoa shaka wananchi na wakazi wa Mkoa  huo kuwa hadi sasa hakuna uhaba wa mafuta  japo kuna changamoto ya ongezeko la bei ya bidhaa hiyo.

Vilevile RC Chalamila ametumia nafasi hiyo kuwataka wanasiasa kuacha kulitumia suala la kuongezeka kwa bei ya mafuta kisiasa kwa suala hilo ni la kidunia kutokana na vita iliyotokea na kusababisha kuongeza bei ya mafuta kwenye Soko la Dunia, mabadiliko ya gharama za uletaji mafuta na mabadiliko ya thamani ya dola huku akisisitiza kuwa Serikali chini ya Rais Dkt Samia inaendelea na mikakati na kuwa na mifumo bora ya kuhifadhi mafuta ili changamoto kama hiyo iwe historia

Aidha Mkuu wa Mkoa Mhe Albert Chalamila amezungumzia ziara ya Waziri Mkuu Dkt Mwigulu Nchemba aliyoifanya wiki iliyopita kwenye soko lililoungua moto la Ubungo simu 2000 na kusema kuwa maelekezo aliuoyatoa yanatekelezwa pamoja na yale ualiyotolewa na waziri wa TAMISEMI

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila amewataka wananchi wa Mkoa huo kujitokeza katika mbio za Mwenge wa Uhuru unaotarajia kuwasili jijini humo aprili 13 mwaka huu ukitokea Mkoa wa Kaskazini Unguja ambapo utakimbizwa umbali wa kilometa 392.22 kwenye Wilaya zote tano za mkoa huo ukikagua, kuzimdua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi 35 yenye thamani ya shilingi bilioni 113.5

Akizungumza na waandishi wa habari RC Chalamila amesema shabaha ya mbio za mwenge wa uhuru ni kuleta umoja, mshikamano na udugu baina ya watanzania ambapo amesema aprili 13 baada ya kuwasili utakimbizwa wilayani Ilala, April 14 wilaya ya Kigamboni, April 15 wilaya ya Temeke, April 16 wilaya ya Ubungo na April 17 wilaya ya Kinondoni na April 18 Mkoa utakabidhi Mkoa wa Pwani.

RC Chalamila amesema Mwengu wa Uhuru kwa mwaka huu wa 2026 umebeba ujumbe wa kudumisha amani, umoja na mshikamano wa kitaifa chini ya kauli mbiu isemayo “Tanzania ni Yetu Sote, Tushikamane kwa Pamoja Kuleta Maendeleo”