Na MWANDISHI WETU
WAZIRI wa Ujenzii, Abdalllah Ulega, amesema serikali itaendelea kushirikiana kikamilifu na wabunifu majengo kuhakikisha kuwa na miji iliyopangika vyema na manengo salama.
Aidha amewataka wabunifu majengo nchini kuwekeza taaluma yao katika ubunifu kwa kutumia teknolojia kubwa lakini kwa gharama nafuu.
Ulega ameyasema hayo, mjini Morogoro, alipofungua semina ya siku mbili ya wabunifu majengo kuhusu upangaji miji na ujenzi wa nyumba bora zinazo zingatia teknolojia ya sasa na zamani (AAT CPD)
Semina hiyo iimeshirkishs wataalamu zaidi ya 300 kutoka ndani na nje ya ncjhi imeandaliwa na Chama cha Wabunifu Majengo Tanzania (AAT)
Waziri Ulega amesema fani ya ubunifu majengo ni fani muhimu hivyo kuwataks wataalamu hao kujitangaza ili jamii iwatambue na kuwatumia.
“Vilevile nyie ni wanasayansi wazuri. Tumieni ubunifu wenu kubuni mambo ya teknolojia kwa gharama nafuu itakayo endana na mahitaji na mazingira ya nchi yetu” amesema Ulega.
Amebainisha katika dunia ya sasa wanasayansi wanatumia teknolojia kubuni vitu kwa gharama nafuu vinavyo weza kuingia katika ushindani na vitu vya teknojia ya gharama kubwa.
“Hivyo nasisitiza mtumie ubunifu wenu katika kuisaidia jamii yetu kwa kutumia teknolojia ya gharama nafuu yenye tija,” amebainisha.
Pia ameitaka AAT kuitangaza taaluma hii kwani wabunifu majengo wakitumika vyema wanasaidia taifa kuwa na miji bora inayoendelea yenye ujenzi salama na iliyopangika.
“Fani yenu ni muhimu lakini imefichwa. Huenda imefichwa zaidi na wahandisi ambao wanafanya kazi zote za ujenzi. Mkijitangaza mkajulikana jamii itawatumia na itaachana pia na kuwatumia vishoka katika ujenzi,” ameeleza Waziri Ulega.
Amebainis serikali chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, itaendelea kushirikiana na wabunifu majengo nchini kwa kuzifanyia marekebisho,sheria na kanuni mbalimbali ili kuketa uwajibikaji bora ma ufanisi.
Aidha ameipongeza AAT kwa kuandaa semina hiyo hasa kuwashirikisha wanafunzi wa vyuo na vyu vikuu wanasomea taaluma mbalimbali za kada hiyo ya ujenzi jambo alilosema litaleta tija kwa taifa.
Awali Rais wa AAT Mack T’Chawi, alisema semina hiyo itasaidia kutoa elimu ya namna ya kupanga miji inayobadilika kullngana na teknolojia ya sasa na ya zamani.
Katibu Mtendaji wa AAT Attie Ally, alisema katika kuunga mkono jitihada za Rais Dk. Samia kukiza sekta ya utalii nchini washiriku wa semina hiyo leo watakwenda kutalii katika Mbuga ya Wanyama ya Mikumi mkoani humo.
“AAT tunaujga mkono jitihada za Rais Dk. Samia za kutangaza utalii, hivyo washiriki wote wa semina hii ya kimataifa tutawapeleka Mikumi kutalii,” almesema Attie.
Washiriki wa semina hiyo wamesema ina tija kubwa kwao katika kubadilishana uzoefu hasa kipindi hiki ambapo miji mingi inaendelea kukua kutokana na ongezeko la watu.


