Kyombo aachiwa msala Napsa Stars

USAJILI wa mshambuliaji wa Kitanzania, Habib Kyombo kwenda Napsa Stars ya Zambia unatajwa kama moja ya sajili zitakazokwenda kuisaidia kumaliza ukata wa mabao kwenye eneo la ushambuliaji.

Napsa iko nafasi ya 16 kati ya 18 kwenye msimamo wa ligi ikicheza mechi 27, imeshinda sita, sare tisa na kupoteza mechi 12 ikikusanya pointi 27.

Ni moja ya timu zilizofunga mabao machache kwenye ligi hiyo, 19 na kuruhusu 28, huku saba yamefungwa na washambuliaji na mengine na mabeki na viungo.

Inaelezwa malengo ya timu ni kusalia ligi kuu na timu imeona changamoto iko kwenye wachezaji hivyo wamesajili wapya ili kuleta changamoto ya waliokuwepo.

Hivyo kusajiliwa kwa Kyombo ni kuja kuiongzezea nguvu timu hiyo kwenye eneo la ushambuliaji ili limefunga mabao kusalia ligi kuu.

Kocha wa timu hiyo, Tennant Chilumba alisema “Tulikuwa na mapungufu maeneo mbalimbali hasa eneo la ushambuliaji tukakaa na uongozi eneo lipi tunapaswa kuliboresha ili tuweze kubaki.”

“Nina imani na Kyombo kwa sababu ni mshambuliaji ambaye anayeweza kuongeza kitu kwenye kikosi na kutusaidia kwa mabao yake kwa kushirikiana na wenzie.”